060 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI (Kwa Wanafunzi Walioko na Wasiokuwepo Shuleni)
1.0 UTANGULIZI
Fomati hii ya Historia ya Tanzania na Maadili kwa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) imezingatia umahiri wa Kidato cha Kwanza na cha Pili kwenye muhtasari wa somo uliotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mwaka 2023. Fomati hii mpya inabadili mtazamo wa tathmini uliozingatia maudhui kwenda kwenye mtazamo unaozingatia umahiri, ukisisitiza kupima uwezo wa juu wa kufikiri kwa wanafunzi, kama inavyosisitizwa kwenye muhtasari uliopo.
2.0 UMAHIRI MKUU
Upimaji utalenga kubaini umahiri wa mwanafunzi katika:
2.1 kulinda historia, urithi na maadili ya taifa;
2.2 kuelewa historia ya jamii za kitanzania na maadili yake kabla ya ukoloni;
2.3 kuelewa historia ya Tanzania na maadili wakati wa ukoloni, 1890 – 1960; na
2.4 kuelewa historia ya ujenzi wa taifa la Tanzania na maadili katika kipindi cha 1961 – 1966.
3.0 MUUNDO WA UPIMAJI
Upimaji utakuwa na karatasi moja (1) na utafanyika kwa muda wa saa 2:30. Upimaji utafanyika kwa saa 2:55 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Karatasi itakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali 10 yenye alama 100. Mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote.
Sehemu A itakuwa na maswali mawili (2). Swali la kwanza litakuwa la kuchagua jibu sahihi na litajumuisha vipengele 10 vyenye alama moja (1) kila moja, hivyo kuwa na jumla ya alama 10. Swali la pili litakuwa la kuoanisha na litajumuisha vipengele vitano (5) vyenye alama moja (1) kila moja, hivyo kuwa na jumla ya alama tano (5). Kwa hiyo, jumla ya alama katika sehemu hii itakuwa ni alama 15.
Sehemu B itakuwa na maswali saba (7) ya majibu mafupi. Mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote, ambapo kila swali litakuwa na alama 10. Hivyo, jumla ya alama katika sehemu hii itakuwa ni alama 70.
Sehemu C itakuwa na swali moja (1) la insha lenye alama 15.
4.0 UMAHIRI UTAKAOPIMWA
Mwanafunzi atapimwa katika umahiri ufuatao:
4.1 Kulinda historia, urithi na maadili ya Taifa.
4.1.1 kuelezea chimbuko la jamii za Kitanzania na maadili yake;
4.1.2 kumudu maarifa na ujuzi wa maadili na urithi wa jamii za Kitanzania;
4.1.3 kutumia maarifa na ujuzi wa historia na urithi kubuni fursa mbalimbali zilizopo katika jamii za Kitanzania; na
4.1.4 kubaini fursa mbalimbali za kujenga ushirikiano na kukuza uchumi wa kitaifa.
4.2 Kumudu historia ya jamii za Kitanzania na maadili yake kabla ya ukoloni.
4.2.1 kuchambua mifumo ya kijamii (elimu, afya, utamaduni) iliyokuza na kuendeleza maadili ya jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni;
4.2.2 kuchambua mifumo iliyokuza na kuendeleza uchumi na siasa katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni; na
4.2.3 kutathmini vichocheo vya mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni.
4.3 Kumudu historia ya Tanzania na maadili wakati wa ukoloni, 1890 – 1960.
4.3.1 kutumia maarifa na ujuzi wa chimbuko na ukuaji wa mfumo wa ukoloni kuelewa uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na mataifa yaliyoitawala;
4.3.2 kutathmini athari za mfumo wa ukoloni kwenye maadili ya jamii za Kitanzania; na
4.3.3 kuchambua jitihada za jamii za Kitanzania kupinga ukoloni na maadili ya kikoloni.
4.4 Kumudu historia ya ujenzi wa taifa la Tanzania na maadili katika kipindi cha 1961 – 1966.
4.4.1 kuchambua mifumo ya uchumi, siasa, utamaduni, jamii na maadili iliyojengwa, 1961-1966; na
4.4.2 kumudu historia ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
5.0 JEDWALI LA KUTAHINI 060 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Umahiri Mkuu 1: Kulinda historia, urithi na maadili ya Taifa
Umahiri Mahususi 1.1: Kuelezea chimbuko la jamii za Kitanzania na maadili yake
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini
Idadi ya Maswali: 5
Asilimia: 26.3%
Umahiri Mahususi 1.2: Kuelewa maarifa na ujuzi wa maadili na urithi wa jamii za Kitanzania
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Umahiri Mahususi 1.3: Kutumia maarifa na ujuzi wa historia na urithi kubuni fursa mbalimbali zilizopo katika jamii za Kitanzania
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Umahiri Mahususi 1.4: Kubaini fursa mbalimbali za kujenga ushirikiano na kukuza uchumi wa kitaifa
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Umahiri Mkuu 2: Kuelewa historia ya jamii za Kitanzania na maadili yake kabla ya ukoloni
Umahiri Mahususi 2.1: Kuchambua mifumo ya kijamii (elimu, afya, utamaduni) iliyokuza na kuendeleza maadili ya jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: 4
Asilimia: 21.1%
Umahiri Mahususi 2.2: Kuchambua mifumo iliyokuza na kuendeleza uchumi na siasa katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Umahiri Mahususi 2.3: Kutathmini vichocheo vya mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Umahiri Mkuu 3: Kuelewa historia ya Tanzania na maadili wakati wa ukoloni, 1890 – 1960
Umahiri Mahususi 3.1: Kutumia maarifa na ujuzi wa chimbuko na ukuaji wa mfumo wa ukoloni kuelewa uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na mataifa yaliyoitawala
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: 7
Asilimia: 36.8%
Umahiri Mahususi 3.2: Kutathmini athari za mfumo wa ukoloni kwenye maadili ya jamii za Kitanzania
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Umahiri Mahususi 3.3: Kuchambua jitihada za jamii za Kitanzania kupinga ukoloni na maadili ya kikoloni
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Umahiri Mkuu 4: Kuelewa historia ya ujenzi wa Taifa la Tanzania na maadili katika kipindi cha 1961 – 1966
Umahiri Mahususi 4.1: Kuchambua mifumo ya uchumi, siasa, utamaduni, jamii na maadili iliyojengwa, 1961-1966
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: 3
Asilimia: 15.8%
Umahiri Mahususi 4.2: Kuelewa historia ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
Idadi ya Maswali: Included above
Asilimia: Included above
Jumla ya Maswali: 19
Jumla ya Asilimia: 100%

MATOKEO YA MITIHANI KIDATO CHA PILI 2025
Post a Comment