021 KISWAHILI (Kwa Wanafunzi Walioko na Wasiokuwepo
Shuleni)
1.0 UTANGULIZI
Fomati hii ya Kiswahili kwa Upimaji wa Kidato cha Pili
(FTNA) imezingatia umahiri za Kidato cha Kwanza na cha Pili kwenye muhtasari wa
somo uliotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mwaka 2023. Fomati hii
inabadili mtazamo wa tathmini unaozingatia maudhui kwenda kwenye mtazamo
unaozingatia umahiri, ukisisitiza kupima uwezo wa juu wa kufikiri kwa wanafunzi
na ujuzi wa vitendo kama inavyosisitizwa katika muhtasari uliopo.
2.0 UMAHIRI WA JUMLA
Upimaji utalenga kubaini umahiri wa wanafunzi katika:
2.1 kutumia maarifa na stadi alizozipata katika hatua ya
elimu ya msingi kuimarisha na kupanua uelewa wa kitaaluma;
2.2 kuthamini uraia na Tunu za Taifa; na
2.3 kutumia ujuzi na stadi kumwezesha mwanafunzi kujiajiri, kuajiriwa na
kuyamudu maisha na mazingira.
3.0 MUUNDO WA KARATASI YA UPIMAJI
Upimaji wa somo la Kiswahili utafanywa kwa muda wa saa 2:30.
Wanafunzi wenye mahitaji maalum watafanya upimaji kwa muda wa saa 2:55.
Karatasi ya Upimaji itakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi
(10), mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote. Upimaji huu utakuwa na jumla ya
alama 100.
Sehemu A itakuwa na maswali mawili (2). Swali la
1 litakuwa la kuchagua na litakuwa na jumla ya alama 10. Swali la 2 litakuwa la
kuoanisha na litakuwa na jumla ya alama 5. Sehemu hii itakuwa na jumla ya alama
15.
Sehemu B itakuwa na maswali saba (7) ya majibu
mafupi. Mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote. Sehemu hii itakuwa na jumla
ya alama 70.
Sehemu C itakuwa na swali moja (1) la insha.
Mwanafunzi atatakiwa kujibu swali hili na litakuwa na jumla ya alama 15.
4.0 UMAHIRI UTAKAOPIMWA
Upimaji utahusisha umahiri ufuatao:
4.1 Kumudu misingi ya Kiswahili:
- 4.1.1
kutambua Kiswahili kama kielelezo cha utaifa na utambulisho wa Mtanzania.
- 4.1.2
kukuza uelewa wa sarufi ya Kiswahili.
4.2 Kumudu lugha ya mazungumzo na ya maandishi.
- 4.2.1
kusikiliza na kuelewa mazungumzo.
- 4.2.2
kusoma matini kwa ufasaha na ufahamu.
4.3 Kuwasiliana katika miktadha mbalimbali.
- 4.3.1
kutumia kamusi katika miktadha mbalimbali;
- 4.3.2
kuwasiliana kwa ufasaha kwa njia ya mazungumzo; na
- 4.3.3
kuwasiliana kwa njia ya maandishi katika miktadha mbalimbali.
5.0 JEDWALI LA UTAHINI WA SOMO LA 021 KISWAHILI
Umahiri Mkuu 1: Kumudu misingi ya Kiswahili
Umahiri Mahsusi 1.1: Kutambua Kiswahili kama
kielelezo cha utaifa na utambulisho wa Mtanzania
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini
- Idadi
ya Maswali: 1
- Asilimia:
2.86%
Umahiri Mahsusi 1.2: Kukuza uelewa wa sarufi ya
Kiswahili
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
- Idadi
ya Maswali: 5
- Asilimia:
27.14%
Umahiri Mkuu 2: Kumudu lugha ya mazungumzo na ya
maandishi
Umahiri Mahsusi 2.1: Kuelewa lugha ya
mazungumzo. Kusoma matini kwa ufasaha na ufahamu
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
- Idadi
ya Maswali: 3
- Asilimia:
17.14%
Umahiri Mkuu 3: Kuwasiliana katika miktadha
mbalimbali
Umahiri Mahsusi 3.1: Kutumia kamusi katika
miktadha mbalimbali. Kuwasiliana kwa ufasaha kwa njia ya mazungumzo
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
- Idadi
ya Maswali: 1
- Asilimia:
5.71%
Jumla ya Maswali: 19
Jumla ya Asilimia: 100%

MATOKEO YA MITIHANI KIDATO CHA PILI 2025
Post a Comment