📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

015 Elimu ya Dini ya Kiislamu Form Two Necta Format 2026

 

015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU (Kwa Wanafunzi Walioko na Wasiokuwepo Shuleni)

1.0 UTANGULIZI

Formati hii ya Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) imezingatia mahiri za Kidato cha Kwanza na cha Pili kwenye muhtasari wa somo uliotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mwaka 2023. Formati hii inabadili mtazamo wa tathmini unaozingatia maudhui kwenda kwenye mtazamo unaozingatia umahiri, ukisisitiza kupima uwezo wa juu wa kufikiri kwa wanafunzi na ujuzi wa vitendo kama inavyosisitizwa katika muhtasari uliopo.

2.0 UMAHIRI MKUU

Upimaji utalenga kubaini umahiri wa mwanafunzi katika:

2.1 kumtambua, kumpenda, kumtukuza na kumsifu Allah (S.W);
2.2 kumtumikia Allah (S.W) katika kila kipengele cha maisha; na
2.3 kulingania na kusimamisha haki na uadilifu katika jamii.

3.0 MUUNDO WA KARATASI YA UPIMAJI

Upimaji wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu utafanywa kwa muda wa saa 2:30. Wanafunzi wenye mahitaji maalum watafanya upimaji kwa muda wa saa 2:55. Karatasi ya upimaji itakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali 10 yenye jumla ya alama 100. Mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote.

Sehemu A itakuwa na maswali mawili (2). Swali la 1 litakuwa la kuchagua majibu sahihi lenye vipengele 10 ambapo kila kipengele kitakuwa na alama moja (1). Swali la 2 litakuwa na vipengele vitano (5) vya kuoanisha ambapo kila kipengele kitakuwa na alama moja (1). Hivyo, sehemu hii itakuwa na alama 15.

Sehemu B itakuwa na maswali saba (7) ya majibu mafupi ambapo kila swali litakuwa na alama 10. Mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote. Hivyo, sehemu hii itakuwa na jumla ya alama 70.

Sehemu C itakuwa na swali moja (1) la insha ambalo litakuwa na alama 15.

4.0 MAHIRI ZITAKAZOPIMWA

Upimaji utahusisha mahiri zifuatazo:

4.1 Kumtambua, kumpenda, kumtukuza na kumsifu Allah (S.W).

  • 4.1.1 kutambua uwepo wa Allah (S.W) na sifa zake;
  • 4.1.2 kuisoma Qur'an kwa Mazingatio ya Hukumu na Ujumbe; na
  • 4.1.3 kuishi kwa kuzingatia Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W).

4.2 Kumtumikia Allah (S.W) katika kila kipengele cha maisha.

  • 4.2.1 kutekeleza nguzo za Uislamu na kuzingatia lengo la kila nguzo; na
  • 4.2.2 kuchunga mipaka ya Allah (S.W) katika kuendesha maisha ya binafsi na jamii.

4.3 Kulingania na kusimamisha haki na uadilifu katika jamii.

  • 4.3.1 kutumia Qur'an na Sunnah kulingania jamii; na
  • 4.3.2 kutumia historia ya Uislamu kujenga mwenendo mwema wa jamii.

5.0 JEDWALI LA UTAHINI WA SOMO LA 15 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

Umahiri Mkuu 1: Kumtambua, kumpenda, kumtukuza na kumsifu Allah (S.W)

Umahiri Mahususi 1.1: Kutambua Uwepo wa Allah (S.W) na sifa zake

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini
  • Idadi ya Maswali: 3
  • Uzito: 15.78%

Umahiri Mahususi 1.2: Kuisoma Qur'an kwa Mazingatio ya Hukumu na Ujumbe

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini
  • Idadi ya Maswali: 4
  • Uzito: 21.05%

Umahiri Mahususi 1.3: Kuishi kwa kuzingatia Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W)

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
  • Idadi ya Maswali: 2
  • Uzito: 10.53%

Umahiri Mkuu 2: Kumtumikia Allah (S.W) katika kila kipengele cha maisha

Umahiri Mahususi 2.1: Kutekeleza nguzo za Uislamu kwa kuzingatia lengo la kila nguzo

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
  • Idadi ya Maswali: 4
  • Uzito: 21.05%

Umahiri Mahususi 2.2: Kuchunga mipaka ya Allah (S.W) katika kuendesha maisha ya binafsi na jamii

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
  • Idadi ya Maswali: 2
  • Uzito: 10.53%

Umahiri Mkuu 3: Kulingania na kusimamisha haki na uadilifu katika jamii

Umahiri Mahususi 3.1: Kutumia Qur'an na Sunnah kulingania jamii

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
  • Idadi ya Maswali: 2
  • Uzito: 10.53%

Umahiri Mahususi 3.2: Kutumia historia ya Uislamu kujenga mwenendo mwema wa jamii

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
  • Idadi ya Maswali: 2
  • Uzito: 10.53%

Jumla ya Maswali: 19
Jumla ya Asilimia: 100%

 

Post a Comment