015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU (Kwa Wanafunzi Walioko na
Wasiokuwepo Shuleni)
1.0 UTANGULIZI
Formati hii ya Elimu ya Dini ya
Kiislamu kwa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) imezingatia mahiri za Kidato cha
Kwanza na cha Pili kwenye muhtasari wa somo uliotolewa na Taasisi ya Elimu
Tanzania (TET) mwaka 2023. Formati hii inabadili mtazamo wa tathmini
unaozingatia maudhui kwenda kwenye mtazamo unaozingatia umahiri, ukisisitiza
kupima uwezo wa juu wa kufikiri kwa wanafunzi na ujuzi wa vitendo kama
inavyosisitizwa katika muhtasari uliopo.
2.0 UMAHIRI MKUU
Upimaji utalenga kubaini umahiri wa mwanafunzi katika:
2.1 kumtambua, kumpenda, kumtukuza na kumsifu Allah (S.W);
2.2 kumtumikia Allah (S.W) katika kila kipengele cha maisha; na
2.3 kulingania na kusimamisha haki na uadilifu katika jamii.
3.0 MUUNDO WA KARATASI YA UPIMAJI
Upimaji wa somo la Elimu ya Dini
ya Kiislamu utafanywa kwa muda wa saa 2:30. Wanafunzi wenye mahitaji maalum
watafanya upimaji kwa muda wa saa 2:55. Karatasi ya upimaji itakuwa na sehemu
A, B na C zenye jumla ya maswali 10 yenye jumla ya alama 100. Mwanafunzi
atatakiwa kujibu maswali yote.
Sehemu A itakuwa na
maswali mawili (2). Swali la 1 litakuwa la kuchagua majibu sahihi lenye
vipengele 10 ambapo kila kipengele kitakuwa na alama moja (1). Swali la 2
litakuwa na vipengele vitano (5) vya kuoanisha ambapo kila kipengele kitakuwa
na alama moja (1). Hivyo, sehemu hii itakuwa na alama 15.
Sehemu B itakuwa na
maswali saba (7) ya majibu mafupi ambapo kila swali litakuwa na alama 10.
Mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote. Hivyo, sehemu hii itakuwa na jumla ya
alama 70.
Sehemu C itakuwa na swali moja (1) la insha
ambalo litakuwa na alama 15.
4.0 MAHIRI ZITAKAZOPIMWA
Upimaji utahusisha mahiri zifuatazo:
4.1 Kumtambua, kumpenda, kumtukuza na kumsifu Allah
(S.W).
- 4.1.1
kutambua uwepo wa Allah (S.W) na sifa zake;
- 4.1.2
kuisoma Qur'an kwa Mazingatio ya Hukumu na Ujumbe; na
- 4.1.3
kuishi kwa kuzingatia Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W).
4.2 Kumtumikia Allah (S.W) katika kila kipengele cha
maisha.
- 4.2.1
kutekeleza nguzo za Uislamu na kuzingatia lengo la kila nguzo; na
- 4.2.2
kuchunga mipaka ya Allah (S.W) katika kuendesha maisha ya binafsi na
jamii.
4.3 Kulingania na kusimamisha haki na uadilifu katika
jamii.
- 4.3.1
kutumia Qur'an na Sunnah kulingania jamii; na
- 4.3.2
kutumia historia ya Uislamu kujenga mwenendo mwema wa jamii.
5.0 JEDWALI LA UTAHINI WA SOMO LA 15 ELIMU YA DINI YA
KIISLAMU
Umahiri Mkuu 1: Kumtambua, kumpenda, kumtukuza
na kumsifu Allah (S.W)
Umahiri Mahususi 1.1: Kutambua Uwepo wa Allah
(S.W) na sifa zake
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini
- Idadi
ya Maswali: 3
- Uzito:
15.78%
Umahiri Mahususi 1.2: Kuisoma Qur'an kwa
Mazingatio ya Hukumu na Ujumbe
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini
- Idadi
ya Maswali: 4
- Uzito:
21.05%
Umahiri Mahususi 1.3: Kuishi kwa kuzingatia
Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W)
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
- Idadi
ya Maswali: 2
- Uzito:
10.53%
Umahiri Mkuu 2: Kumtumikia Allah (S.W) katika
kila kipengele cha maisha
Umahiri Mahususi 2.1: Kutekeleza nguzo za
Uislamu kwa kuzingatia lengo la kila nguzo
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
- Idadi
ya Maswali: 4
- Uzito:
21.05%
Umahiri Mahususi 2.2: Kuchunga mipaka ya Allah
(S.W) katika kuendesha maisha ya binafsi na jamii
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
- Idadi
ya Maswali: 2
- Uzito:
10.53%
Umahiri Mkuu 3: Kulingania na kusimamisha haki
na uadilifu katika jamii
Umahiri Mahususi 3.1: Kutumia Qur'an na Sunnah
kulingania jamii
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
- Idadi
ya Maswali: 2
- Uzito:
10.53%
Umahiri Mahususi 3.2: Kutumia historia ya
Uislamu kujenga mwenendo mwema wa jamii
- Ujuzi:
Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kunuda
- Idadi
ya Maswali: 2
- Uzito:
10.53%
Jumla ya Maswali: 19
Jumla ya Asilimia: 100%

MATOKEO YA MITIHANI KIDATO CHA PILI 2025
Post a Comment