📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

021 Kiswahili Form Two Necta Format 2026

 

021 KISWAHILI (Kwa Wanafunzi Walioko na Wasiokuwepo Shuleni)

1.0 UTANGULIZI

Fomati hii ya Kiswahili kwa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) imezingatia umahiri za Kidato cha Kwanza na cha Pili kwenye muhtasari wa somo uliotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mwaka 2023. Fomati hii inabadili mtazamo wa tathmini unaozingatia maudhui kwenda kwenye mtazamo unaozingatia umahiri, ukisisitiza kupima uwezo wa juu wa kufikiri kwa wanafunzi na ujuzi wa vitendo kama inavyosisitizwa katika muhtasari uliopo.

2.0 UMAHIRI WA JUMLA

Upimaji utalenga kubaini umahiri wa wanafunzi katika:

2.1 kutumia maarifa na stadi alizozipata katika hatua ya elimu ya msingi kuimarisha na kupanua uelewa wa kitaaluma;
2.2 kuthamini uraia na Tunu za Taifa; na
2.3 kutumia ujuzi na stadi kumwezesha mwanafunzi kujiajiri, kuajiriwa na kuyamudu maisha na mazingira.

3.0 MUUNDO WA KARATASI YA UPIMAJI

Upimaji wa somo la Kiswahili utafanywa kwa muda wa saa 2:30. Wanafunzi wenye mahitaji maalum watafanya upimaji kwa muda wa saa 2:55. Karatasi ya Upimaji itakuwa na sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10), mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote. Upimaji huu utakuwa na jumla ya alama 100.

Sehemu A itakuwa na maswali mawili (2). Swali la 1 litakuwa la kuchagua na litakuwa na jumla ya alama 10. Swali la 2 litakuwa la kuoanisha na litakuwa na jumla ya alama 5. Sehemu hii itakuwa na jumla ya alama 15.

Sehemu B itakuwa na maswali saba (7) ya majibu mafupi. Mwanafunzi atatakiwa kujibu maswali yote. Sehemu hii itakuwa na jumla ya alama 70.

Sehemu C itakuwa na swali moja (1) la insha. Mwanafunzi atatakiwa kujibu swali hili na litakuwa na jumla ya alama 15.

4.0 UMAHIRI UTAKAOPIMWA

Upimaji utahusisha umahiri ufuatao:

4.1 Kumudu misingi ya Kiswahili:

  • 4.1.1 kutambua Kiswahili kama kielelezo cha utaifa na utambulisho wa Mtanzania.
  • 4.1.2 kukuza uelewa wa sarufi ya Kiswahili.

4.2 Kumudu lugha ya mazungumzo na ya maandishi.

  • 4.2.1 kusikiliza na kuelewa mazungumzo.
  • 4.2.2 kusoma matini kwa ufasaha na ufahamu.

4.3 Kuwasiliana katika miktadha mbalimbali.

  • 4.3.1 kutumia kamusi katika miktadha mbalimbali;
  • 4.3.2 kuwasiliana kwa ufasaha kwa njia ya mazungumzo; na
  • 4.3.3 kuwasiliana kwa njia ya maandishi katika miktadha mbalimbali.

5.0 JEDWALI LA UTAHINI WA SOMO LA 021 KISWAHILI

Umahiri Mkuu 1: Kumudu misingi ya Kiswahili

Umahiri Mahsusi 1.1: Kutambua Kiswahili kama kielelezo cha utaifa na utambulisho wa Mtanzania

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini
  • Idadi ya Maswali: 1
  • Asilimia: 2.86%

Umahiri Mahsusi 1.2: Kukuza uelewa wa sarufi ya Kiswahili

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
  • Idadi ya Maswali: 5
  • Asilimia: 27.14%

Umahiri Mkuu 2: Kumudu lugha ya mazungumzo na ya maandishi

Umahiri Mahsusi 2.1: Kuelewa lugha ya mazungumzo. Kusoma matini kwa ufasaha na ufahamu

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
  • Idadi ya Maswali: 3
  • Asilimia: 17.14%

Umahiri Mkuu 3: Kuwasiliana katika miktadha mbalimbali

Umahiri Mahsusi 3.1: Kutumia kamusi katika miktadha mbalimbali. Kuwasiliana kwa ufasaha kwa njia ya mazungumzo

  • Ujuzi: Kukumbuka, Kuelewa, Kutumia, Kuchambua, Kutathmini, Kutunda
  • Idadi ya Maswali: 1
  • Asilimia: 5.71%

Jumla ya Maswali: 19
Jumla ya Asilimia: 100%

 

Post a Comment